Course Purpose

Lengo kuu la moduli hii ni kukusaidia kuelewa tanzu tofauti za kifasihi,maudhui ya aina mbali mbali na mitindo mbali mbali ya matumizi ya lugha katika kazi mbali mbali za kifasihi.Uchambuzi wa kazi za kifasihi utafanywa kwa kutumia nadharia mbali mbali ili kukuwezesha kuelewa tanzu tofauti kikamilifu.

 

 

Course Learning Outcomes

CLO 1: Nadharia kuu za fasihi na namna zinavyotumika katika uhakiki wa Fasihi ya Kiswahili

CLO 2: Kuhakiki kazi za kifasihi za Kiswahili na kutambua maudhui, motifu na lugha ya kitamathali kama ilivyotumika

CLO 3: Kutumia mielekeo ya kinadharia katika uhakiki wa kazi za Kifasihi kwa kuzitegemeza vipindi vya kihistoria na miktadha ya kijamii

CLO 4: Kuelewa tanzu tofauti za Fasihi ya Kiswahili na njia mwafaka za kuzihakiki.

 

Course Content

Nadharia ni istilahi inayotumiwa kurejelea kauli au kaida za kujumla zinazotegemezwa kwenye uwazaji fulani. (Wamitila2003).Nadharia hasa hutumika kueleza mambo ya kitaaluma kwa njia ambayo ni razini badala ya kutumia hisia. Kwa kawaida nadharia huwa na nguzo zake kuu ambazo hutegemewa katika kueleza finomena fulani. Ni muhimu kutambua kuwa kuna haja ya kuwa makini katika kutambua nadharia mwafaka ambayo inaweza kutumika kikamilifu katika uchambuzi wa finomena fulani.

Kwa upande mwingine uhakiki ni uchunguzi wa finomena fukani kwa nia ya kuielewa kikamilifu. Mchakato huu unaweza kuhusisha kugawanya dhana kubwa katika vijisehemu vyake vidogo vidogo kwa nia ya kuelewa dhana yenyewe kwa ukamilifu.